LIJUE BARAZA LAKO-BAKWATA

BARAZA KUU LA WAISLAMU WA TANZANIA - BAKWATA NATIONAL MOSLEM COUNCIL OF TANZANIA المجلس الأعلى للشئون الإسلامية بتنزانيا

Monday, July 10, 2006

Mufti Simba angurumia kiwanja cha Chang'ombe

Mufti Simba angurumia kiwanja cha Chang'ombe

*Alonga ni cha BAKWATA, awawajibisha vigogo 7


MUFTI wa Tanzania Sheikh Mkuu, Sheikh Issa Bin Shaaban Simba, ameiomba Serikali irudishe kiwanja cha Waislamu kilichopo Chang'ombe, Dar es Salaam, kwani mikataba iliyotumika kukiuza ni ya kughushi.

Hayo aliyasema Dar es Salaama jana, baada ya kukabidhiwa taarifa na Tume ya watu watano aliyoiunda kwa ajili ya kufuatilia mgogoro wa kiwanja hicho kilichopo Wilaya ya Temeke.

Katika kupokea taarifa hiyo, Sheikh Mkuu, alitangaza pia kuwawajibisha viongozi saba waandamizi wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), kwa kujihusisha na kusaini mikataba batili.

"Mikataba yote iliyosainiwa ili kuhalalalisha uuzwaji wa kiwanja hicho ni ya kughushi, si sahihi kwani zilitumika nembo za kughushi, tuna imani Serikali itatusikiliza," alisema Sheikh Mkuu Simba.

Alisema kwa mujibu wa ripoti ya Tume hiyo, anayo imani kuwa imefanya kazi yake kwa makini na anakubaliana na uamuzi uliofanywa na Halamashauri Kuu ya BAKWATA kwa kuwawajibisha viongozi waliojihusisha na tuhuma hizo.

Tume hiyo iliyokuwa ikiongozwa na Sheikh Sharif Idris Omar, ilimkabidhi majina ya viongozi wanaotuhumiwa kuhusika na kashfa hiyo ya kuandika mikataba batili kuwa ni, Katibu Mkuu wa BAKWATA Alhaj Abas Kihemba, Naibu Katibu wake kwa upande wa mambo ya Dini, Bw. Mussa Hemed.

Wengine waliokumbwa na fagio la Tume hiyo, ni pamoja na Katibu wa Wilaya ya Kinondoni, Bw. Rajabu Mndewa, wadhamini wawili Alhaji Seif Momba na Seif Swai, Imam wa Msikiti wa Alfaruk Sheikh Ali Mbaraka, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa BAKWATA Alihaji Suleiman Mwenda.

Katika tamko hilo, Sheikh Mkuu aliwahakikishia wajumbe wa Tume hiyo na Waislamu wote kwamba kazi ya kwanza ya Tume imemalizika, lakini bado itaendelea na majukumu ya kufuatilia kwa karibu mambo yanayofanywa na viongozi wa BAKWATA na shughuli nyingine zinazofanywa na Waislamu kote nchini.

Tume hiyo iliundwa kwa lengo la kufuatilia uuzwaji wa kiwanja cha Waislamu kilichopo Chang'ombe, ambacho kina ukubwa wa heka 22.7 kinachomilikiwa na BAKWATA tangu mwaka 1968 na ilitakiwa kutoa taarifa ndani ya siku 21.

2 Comments:

 • At 6:01 AM, Blogger Twaha Salum said…

  TUUNGANE ILI KIIPATA NGUVU BAKWATA
  MIMI TWAHA SALUM WA SHINYANGA
  (0767640447)

   
 • At 6:02 AM, Blogger Twaha Salum said…

  matari TOENI MIONGONI MWA VILE MUMEZUKIWA NA ALLAH

   

Post a Comment

<< Home